Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kugharamia Fursa ya Elimu Duniani (UN Education Commission on Financing Global Education Opportunity) amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Haile Mariam Desale alipomtembelea ofisini kwake jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Katika nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu amemkabidhi Waziri Mkuu wa Ethiopia Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation). Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja (miaka 30). Azma kuu ya Mpongo huo ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanaopata elimu iliyo bora na kwa kiwango kinachofanana dunia nzima.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kwa sasa, hali ya elimu katika nchi zinazoendelea inalingana na ile ambayo nchi zinazoendelea zilikuwapo miaka 70 iliyopita. Aidha, ripoti inasisitiza kuwa, ikiwa nchi zinazoendelea zitaendelea kwa kasi ya sasa, itazichukua nchi hizo kati ya miaka 90 na 110 kufikia viwango vya sasa vya nchi zilizoendelea.
Kwa ajili hiyo, Kamisheni inapendekeza njia mpya na bora za kufanya mageuzi katika elimu ikiwemo kuongeza usimamizi, kupanua fursa, kuingiza ubinifu na teknolojia na kuongeza uwekezaji katika elimu kwa kushawishi ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa na Sekta Binafsi. Iwapo mapendekezo hayo yatatekelezwa, nchi zinazoendelea zinaweza kufikida pengo hilo ndani ya miaka 30 ijayo.
Rais Mstaafu ameiomba Ethiopia kujiunga na Mpango huo ambapo Waziri Mkuu wa Ethiopia ameelezea nia ya nchi yake kujiunga na Mpango huo. Ethiopia ni moja kati ya nchi za Afrika ambayo imepiga hatua kubwa katika utoaji wa fursa ya elimu kwa watoto na vijana wake. Pamoja na mafanikio makubwa bado zipo changamoto zinazohitaji hatua madhubuti ili kufikia lengo la kizazi cha elimu ifikapo 2040.
Ziara ya Rais Mstaafu itamfikisha katika nchi 14 barani Afrika ambapo zimechaguliwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo. Tayari amekwishazitembelea nchi za Uganda na Malawi na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi hizo.
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mheshimiwa Haile Mariam Desale, Waziri Mkuu wa Ethiopia jijini Addis Ababa.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkabidhi Ripoti ya Kamisheni ya Elimu Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile Mariam Desale jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mheshimiwa Haile Mariam Desale, Waziri Mkuu wa Ethiopia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...