Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara yake ya kushtukiza katika Jimbo lake kukaguwa miradi ya kimaendeo, December 9 amezunguka katika Zahanati na Shule za Secondary Chalize pamoja na mradi wa ufugaji kuku katika Kata ya Msoga ili kuona utendaji kazi pamoja na miradi ambayo inafanyika pia kuzichukua changamoto zilizopo na kuangalia jinsi ya kuzitatua.
Mh Mbunge Ridhiwani alitembelea katika Hospital ya Msoga ambayo ilijengwa na Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kupitia Ofisi ya Mbunge walitoa vifaa tiba katika Hospital hiyo ikiwamo X-RAY machine, Ado sound Mashine, Vitanda 70,Bed cover, Vitanda zaidi ya 70, mashine za dawa za usingizi zaidi ya tano, mafriji ya kuifadhia damu matatu, kiti kwa ajili ya tiba ya meno na vifaa vingine vingi.

Hospital ya Msoga inatarajiwa kuwa ya wilaya baada ya kukamilisha baadhi ya vitu ikiwemo samani, inaupungufu wa mabenchi ya kukalia wagonjwa 150, viti 150, Meza 40, na Mashelfu ya kuifadhia dawa pamoja na AC katika chumba hicho kwa ajili ya kuifadhia dawa, Ukosefu wa kichomea taka hatarishi pamoja na Mochwari Lakini pia kuna changamoto ya umaliziaji wa chumba cha kuifadhia digital x-ray machine ambayo ni kubwa iliyotolewa na Mh Mbunge
Chumba cha Darasa la Kompyuta katika Shule ya Sekondari Lugoba
Mh Mbunge akiwa katika eneo ambalo litajengwa tank kubwa la maji litakalo sambaza maji mji mzima wa chalize kutokea Ruvu.
Uchimbaji na Uwekaji maboba ya maji kutokea Ruvu kuja Chalinze ukiendelea.
Mh Mbunge akiwa anapewa maelekezo baada kutembelea eneo la ujenzi wa Kiwanda cha uchakataji matunda
Nyumba za walimu zikiwa zimemalizika katika Shule ya Secondari Merento

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...