Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete Desemba 8, 2016 amafanya ziara katika vijiji vya jimbo lake kukagua Miradi ya kimaendeo na kuona namna utekelezaji wake, Katika kijiji cha Kwakonje Shule ya msingi kulikuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya Madarasa lakini tayari ujenzi umeanza katika shule hiyo pamoja na Shule ya Msingi Kibindu, Mbali na Shule katika vijiji hivi changamoto nyingine kubwa ni Maji pamoja na Barabara lakini kupitia Mbunge wao, tayari wamerekebisha barabara ya kutoka Kwaruhombo kwenda kwa Mduma ambayo ni KM 8 iliyokuwa kero kubwa na wamechimba visima kwa msaada wa waturuki katika kijiji cha Kwamsanje lakini pia kutokana na mvua kutonyesha vizuri mwaka jana katika vijiji hivyo kuna changamoto ya uhaba wa chakula lakini kupitia ofisi ya mbunge ziliombwa tan 1200 katika ofisi ya Waziri Mkuu maafa na zikapatikana tan 200 kwa awamu ya kwanza lakini sasa zimepatikana tan 400 na chakula hicho kitagawiwa.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na wanakijiji wa Kibindu katika mkutano baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.
  
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifungua mani katika kisima kilichojengwa kwa msaada wa watu wa Uturuki kupitia Ofisi ya Mbunge katika kijiji cha Kwamsanje baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...