Shirika la Ndege la RwandAir  jana Disemba 1, 2016 lilipokea ndege nyingine mpya aina ya Airbus A330-300 series yenye uwezo wa kubeba abiria 274, na kufikia idadi ya ndege 11 zote zikiwa na ubora wa Kimataifa.

Ndege hizo mpya zina uwezo wa kutoa hudama ya WiFi wakati wote wa safari  na zinauwezo wa kubeba mizigo mingi na mikubwa kuzingatia taratibu za usafirishaji.  
Meneja Mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Ibrahim Bukenya amesema kuwa Shirika hilo kuanzia Disemba 8, 2016 litaongeza safari zake kutokea Dar es Salaam kwenda Kigali mara mbili kwa siku na kuunganisha sehemu mbali mbali hapa Duniani.

Bukenya ameendelea kwa kuwashukuru wadau na washirika wa Shirika hilo kwa kuendelea kuliamini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...