WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amewataka watumishi wa umma kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, sambamba na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma, Simbachawene amesema watumishi hao wanatakiwa kuwa na utendaji unaojali matokeo na kuepuka utendaji wa mazoea.

Amesema wanatakiwa kuzingatia nidhamu na utendaji wa Watumishi wa Umma,na watambue maadili ni nguzo muhimu ya kuepuka vitendo vya ubadhilifu na rushwa mahali pa kazi.

Hata hivyo, amesema kwasasa inafanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa kwenye ofisi hiyo zinazotokana na uhamisho, upangaji wa walimu na michakato ya teuzi mbalimbali.

Waziri huyo amesema kumekuwa na tuhuma kwa baadhi ya watumishi kujihusisha na vitendo vya rushwa na kwamba watumishi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
                   
Sambamba na hilo, ametaka kila Idara na kitengo kuhakikisha kuwa zinapunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuelekeza rasilimali fedha katika kutekeleza majukumu ya msingi ambayo yataleta tija kwa Taifa.

Simbachawene amewaambia wafanyakazi hao kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Viongozi wa juu na kuwatumikia wananchi kwa kupunguza changamoto zilizo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, mara baada ya Waziri wa Nchi kushoto kwake George Simbachawene  kutoa hotuba yake kwa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi George Simbachawene akitoa hotuba kwa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wanaounda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...