Kufuatia Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Jenerali (Mst) George Marwa Waitara
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA
tarehe 29 Oktoba, 2016, Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Profesa
Jumanne A. Maghembe (Mb) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo kwa
mujibu wa Sheria ya Uanzishwaji wa TANAPA Sura ya 282 Jedwali la Pili ikisomwa
pamoja na kifungu cha 8(1)(b) cha Sheria hiyo.
1)
Bi.
Devotha Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Bodi ya Utalii Tanzania.
2) Dkt. Lucy Lugwisha, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira.
3)
Kamishina
Marijan M. Sato, Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Makao
Makuu Jeshi la Polisi.
4)
Profesa Alexander Songorwa, Mkurugenzi wa Wanyamapori kutoka
Wizara ya Maliasili na Utalii.
5)
Profesa Wineaster Anderson, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Maliasili na Utalii Endelevu Afrika (NARESTi Africa).
6)
Bw. George Fumbuka, Mhasibu aliyethibitishwa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti
wa Kampuni ya CORE Securities.
7) Dkt. Chanasa Mpelumbe Ngeleja, Daktari Mkuu wa Mifugo,Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi.
8) Bw. Allan J. H. Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Uteuzi wa
Mwenyekiti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 29/10/2016 hadi tarehe 28/10/2019.
IMETOLEWA
NA:
Maj.
Gen. Gaudence S. Milanzi
KATIBU
MKUU
WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII
30
Novemba, 2016.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...