Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 14, leo Desemba 4, 2016 inaanza kambi rasmi katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Vijana hao 22, wanaingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli unaotarajiwa kufanyika Desemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao una baraka za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), umepangwa kufuata taratibu zote za kimataifa ikiwa ni pamoja na kupigiwa Nyimbo za Taifa kwa timu zote sambamba na kupandisha Bendera za Mataifa husika.
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinatarajiwa kuwa na michezo minne ya kirafiki ya nyumbani kabla ya kucheza na Shelisheli.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...