Afisa
Mawasiliano wa Udart, Deus Buganywa akizungumza na waandishi habari
hawapo pichani juu ya utoaji huduma ya usafiri katika jiji la Dar es
Salaam, leo.
Abiria wakiwa katika Kituo cha mabasi yaendayo Haraka leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Kampuni ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam (UDART) imesema kuwa itaendelea kutoa huduma bora ya usafiri kadri ya uwezo wao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mawasiliano wa Udart
, Deus Buganywa amesema nia ya kampuni ni kuona wananchi wa jiji la Dar
es Salaam wanapata huduma usafiri ulio bora.
Deus
amesema kampuni imekuwa ikipokea maoni mbalimbali ya wananchi na kuweza
kufanyia kazi katika masuala ua utoaji huduma ya usafiri.
Amesema
abiria ni kiungo kikubwa kwao katika kuwasafirisha kutoka sehemu moja
na kwenda nyingine bila usumbufu huku mifumo mingine ikiendeleaa
kuimarishwa ukiwemo wa matumizi ya kadi.
Aidha
amesema wanafunzi sasa wamekuwa na usafiri wa uhakika pasipo kupata
unyanyasaji wowote ambao unaweza kufanya achukie shule kutokana na adha
ya usafiri.
Amesema
mabasi yaliyopo na mahitaji ya abiria hayatoshi wataendelea kuongeza
ili wananchi kuwa na uhakika wa safari zao na kuweza kuleta maendeleo ya
nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...