Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Massaun amewahimiza viajana nchini kushiriki michezo ili kuinua vipaji vitakavyowezesha Tanzania kupata wachezaji wazuri watakaoliwakilisha vyema taifa katika michezo ya kimataifa.

Massaun alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kilele cha michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana ya jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park  ambacho kinahudumia vijana katika michezo mbalimbali.

Massaun alisema ikiwa wazazi watawasimamia vyema watoto wao katika michezo tangu wakiwa wadogo basi hapo baadaye nchi yetu itakuwa na wachezaji wengi ambao wataiwakilisha vyema nchi katika masdhindano mbalimbali.

“Katika nchi nyingine wachezaji wakubwa hawakuibukia ukubwani, walianza kujiimarisha tangu udogo wao na ndio maana wanafanya vizuri hivyo na sisi tujielekeze huko ili tuwe  na wachezaji bora kama wao na serikali itaendelea kutoa msaada wa kila aina unaohitajika ili kufanisha azma hiyo ” Alisema Massaun.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park Bw. Ray Power alisema misaada itakayopatikana kutokana na michezo hiyo ya hisani itatumika kuwaendeleza vijana wadogo waliopo katika kituo hicho ambacho kimejumuisha michezo mbalimbali.

Katika kilele hicho Naibu Waziri Massaun alitoa zawadi mbalimbali kwa washindi katika michezo tofauti iliyoshirikishwa ikiwemo mpira wa miguu, tenesi, magongo na gofu. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akisalimiana na wachezaji wa timu ya watoto kutoka shule ya IST ya jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya watoto kutoka shule ya IST (wenye jezi za blue) na timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy (wenye jezi nyeusi) kabla ya mchezo wao wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akimkabidhi kombe la ushindi nahodha wa timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy baada ya kuibuka mabigwa katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...