Wananchi Wilayani Handeni wametakiwa kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kujihahakikishia huduma bora za jamii.
  
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akisikiliza kero za wananchi wa Kata ya Segera iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni jana katika maadhimisho ya  siku ya Maadili na Haki za Binanadamu Kiwilaya yaliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

Gondwe alisema “ Maadli ni imani njema, sehemu yoyote yenye maadili haki za binadamu hufuatwa, hakuna ardhi itakayouzwa kiholela, wagonjwa watatibiwa vizuri kwenye vituo vya afya, wageni wataingia kwenye maeneo yetu kwa kufuata taratibu za nchi na shughuli zote zitafanyika kwa misingi ya Haki”.

Aidha aliwataka watumishi wa umma na wananci kwa ujumla kufuata sheria, taratibu na kanuni pasipo kujali wala kubagua rangi au cheo cha mtu yeyote. Alisema kuwa Rushwa ni adui wa haki  na kuwataka kuikataa kwa kauli na vitendo.

Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Handeni alivunja baraza la Ardhi la Kata kwa kulalamikiwa na wananchi kutotekeleza maajukumu yeke na kuwaagiza TAKUKURU Wilaya ya Handeni kulichunguza hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari 2017, na mapungufu yoyote yatakayobainika basi hatua za kisheria  zichukue mkondo wake maramoja.

Vilevile aliwaaagiza  Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa kwenye msitu wa hifadhi ya kijiji

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliwataka Maafisa Watendaji na wenyeviti wa Vijiji kusimamia miradi yote ya maendeleo kwa  maadili na uadilifu kutokana na dhamana kubwa waliyonayo kwenye maeneo yao ya kiutawala. Vilevile aliwataka  kusoma tarifa za mapato na matumizi na kuwa tayari kujibu hoja za wananchi kuhusu taarifa za mapato na matumizi. “Mtendaji atakayeshindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi atakua amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake” Alisema Makufwe.

Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima, alisema TAKUKURU itaendelea kupambana na Rushwa kikamilifu na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya Rushwa. Aliwataka wananchi kufichua vitendo vya rushwa vinapotokea au dalili za vitendo hivyo ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu hufanyika kila tarehe 10 Disemba Kitaifa, na Wilayani hapa yalifanyika tarehe 8 Disemba  kutokana na Muingiliano wa Majukumu yakiongozwa na kauli mbiu isemayo.

kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa”.

Alda  Sadango
Afisa habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

9 Desemba 2016.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe, wakisalimia wananchi wa Kata ya Segera
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni  BW. William Makufwe akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho.
 Baadhi ya Maafisa wa TAKUKURU, Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya. 

Baadhi ya wananchi wa kata ya Segera . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...