Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema wanayoyafanya, kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTILES kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W).
Akizungumza  katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Alhaji Mwinyi amesema  kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa akifunga kila siku ya Jumatatu ikiwa ni ishara ya kusherekea siku aliyozaliwa.
 Hivyo ni vyema kuiga mfano huo wa kufanya matendo mema kwa kuyarudia mara kwa mara na kuyadumisha, huku akipongeza uongozi wa NIDA kwa kuwaalika na kusherekea pamoja kwani amejifunza mengi kupitia mawaidha yaliyotolewa na viongozi wa dini waliohutubia akiwemo Sheikh Ally Basaleh.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali akiwemo Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Gharib Bilal, Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Naibu Waziri Wizara ya Afya Hamis Kigwangala, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega. Viongozi wa dini waliokuwepo ni pamoja na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili  Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na  viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali juu ya watanzania  kuyafanyia muendelezo wa yale mema kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTILES kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akizungumza na  viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali katika kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
 Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza machache katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...