Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Ligi kuu ya Vodacom  imeendelea leo katika viwanja mbali mbali huku katika mchezo wa uliozikutanisha  timu ya Azam Fc na Mbeya City ukimalizika kwa suluhu ya timu hizo kushindwa kufungana.
Katika mchezo huo ambao ulianza saa moja usiku katika uwanja wa Chamazi Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa aina yake kwa timu zote zikishambuliana kwa vipindi na kucheza kwa kujiamini na kujituma kuhakikisha wanajaribu kupata ushindi lakini bahati aikuwa upande wowote.
Katika mchezo huo ambao mbeya City imeweza kucheza na wachezaji wawili  ambao washawahi kuchezea timu ya Azam  ambao ni Mrisho Ngassa na Zahoro Pazi  na kuonyesha kuwa mwiba kwa timu hiyo kwa kujaribu kulishambulia lango la timu yao ya zamani mara kadhaa.
Mrisho Ngassa ambaye ameingia katika kipindi cha pili mara baada ya kutoka kwa Tito Okelo ameweza kufanya mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji kwa kuwa tishio katika lango la Azam Fc.

Ngasa ambaye ameweza kucheza kwa kuonyesha uzoefu wa hali ya juu kwa kuweza kusaidia upande wa kati  na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki kutokana na staili yake ya mchezo .
Kikosi cha Mbeya City kilichoanza leo
Kikosi cha Azam Fc.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...