Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara ameliomba baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Mkurugenzi kubuni vyanzo ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa kwa ukusanyaji mapato ipasavyo.

Pia aliwaomba Madiwani wa upinzani kuacha tabia ya kupinga rasimu ya pendekezo la bajeti iliyopendekezwa ya mwaka 2017-2018 pasipokuwa na hoja ya msingi ikiwa ni pamoja na kupinga kodi ya majengo ya kila mwananchi kuchangia kiasi cha shilingi 5000 kwa mwaka hali inayopelekea halmashauri hiyo kushindwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato.

Rai hiyo aliitoa Jana (Leo) katika kikao cha baraza la madiwani cha kuipitia na kupitisha rasimu ya bajeti inayo pendekezwa na balaza hill ambapo Ndagara aliwaomba madiwani kuwashawishi Wananchi kuchangiq shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia Ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuchangia michango mingine iliyopendekezwa kwenye rasimu ilikufikia lengo la kukusanya mapato kwa asilimia 80%.

Aidha Ndagara aliwaomba madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ilikuepuka viporo vilivyo baki kwa bajeti ya mwaka uliopitq ambapo halmashauri hiyo ilishindwa kufikia lengo na kukusanya mapato kwa asilimia 28% kutokana na kukosekana kwa vyanzo vipya vya mapato katika Wilaya.

"Ushauri wangu katika baraza hili kwenye hii bajeti mlio ipitisha nilazima kuwa na vipaumbele ilikuepuka hivi vipolo vilivyo baki niungane na Afisa mipango, tuwqshirikishe Wananchi kwa nguvu kubwa na tuache kuitegemea serikali siku zote lazima tukusanye kodi ilikuweza kuipatia halmashauri mapato kuacha kuweka vipingamizi visivyo kuwa na msingi ", alisema Kanali Ndagara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Lusubiro Mwakabibi aliwaomba madiWani kuikataa bajeti kwa hoja ya msingi, kupinga suala la kila mwananchi kuchangia shilingi 5000 kwa mwaka ni kupinga maendeleo hakuna mwananchi anaeweza kukosa kiasi hicho cha hela kwa mwaka suala la msingi tuongeze vyanzo vya ukusanyaji wa mapato.

Mwakabibi alisema Madiwani wanatakiwa kuwaelimisha Wananchi juu ya ulipaji modi na kuchangia mapato ya serikali, halmashauri ya kakonko ni halmashauri ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato nchini kutokana na vyanzo vidogo vya ukusanyaji mapato halmashauri baada ya kuliona hill imeandaa vyanzo vipya vya mapato ilikuhakikisha mapato yanaongwezeka.

Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya Kakonko Juma Maganga alisema halmashauri imeandaa bajeti ya shilingi bilioni 29.7 iliyopitishwa na madiwani ya mwaka wa fedha 2017 -2018 itakayo husisha makusanyo ya mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali kuu itakayo saidia kukamilisha shuguli za maendeleo ya halmashauri hiyo.


MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara akizungumza kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,katika suala zima la kupanga mkakati mpya wa kubuni vyanzo vya mapato ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa.
 Baadhi ya Madiwani wakiwa kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara alipokuwa akizungumza nao mapema jana katika suala zima la mkakati mpya wa kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...