Imeelezwa kuwa sababu za kihistoria, mila na desturi za jamii ni moja ya changamoto zinazoikabili sekta ya ujenzi kwenye ushirikishaji wa wanawake katika utekelezaji wa miradi ya barabara nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi ),Eng. Joseph Nyamhanga wakati akizindua mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara ambapo Serikali imekuja na mikakati mbalimbali ya kuwashirikisha wanawake katika miradi ya ujenzi wa barabara
"Maandalizi ya mwongozo huu ni sehemu ya mkakati wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika utekelezaji wa mikakati mbalimbali iliyojiwekea ili kuinua maisha ya wanawake kiuchumi,'' amesema Eng. Nyamhanga.

Eng. Nyamhanga ameongeza kuwa utekelezwaji wa mwongozo huo ni moja ya kichocheo cha kuwawezesha wanawake kutoa mchango mkubwa zaidi kuchumi nchini ambapo kwa sasa sekta ya ujenzi inachangia asilimia 13.6 kwenye pato la Taifa.

Aidha ametanabaisha kuwa kwa mwaka 2014/15 kumekuwa na ongezeko la ushiriki wa wanawake katika miradi ya barabara wa uwiano wa kila wahandisi 100 wanaume wanawake 6 ambao kwenye usimamizi wa miradi uwiano ukiwa ni asilimia 6.

Kwa upande wake MKurugenzi wa Idara ya Barabara, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Ujenzi, Eng. Ven Ndyamukama amesema ushirikishwaji wa wanawake katika sekta  ya ujenzi ulianza mwaka 1992 kwa kutekelezwa kwenye mikoa ya Mbeya, Tanga, Shinyanga, Mwanza na Mtwara.

"Kama Wizara tuliona umuhimu wa kuanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kuhakikisha tunawawezesha wanawake katika kazi za ujenzi na hili limesisitizwa hata kwenye sheria ya Ujenzi ya mwaka 2003 (CIP, 2003) kwa kuhakikisha wanawake wanashirikishwa katika kazi za ujenzi ili kuwainua kiuchumi' amesema Eng. Ndyamukama.

Ameongeza kuwa pamoja na mwongozo huu Wizara imeendelea kuwawezesha wanawake kwenye mafunzo mbalimbali ya ujenzi kupitia vyuo mbalimbali vilivyo chini ya wizara na taasisi binafsi.

Takwimu Kutoka Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) zinaonesha kwa mwaka 2014, kati ya jumla ya wahandisi 13,148 waliopo nchini wahandisi wanawake ni 926 ambao ni sawa na asilimia 6.5 wakati kati ya Makampuni ya makandarasi 8,071 yaliyosajiliwa ni makampuni 253 yanamilikiwa na wanawake sawa na asilimia 3.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa maelezo kwa Wadau wa masuala ya Ujenzi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa maelezo kwa katika Wadau wa masuala ya Ujenzi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wananwake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikihwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa barabara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng Ven Ndyamkama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga katika picha ya pamoja na wajumbe wa maendeleo ya sekta ya ujenzi mara baada ya kuzindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho  ya taifa jijini Dar es salaam. Picha na Wizara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...