Na Augustino Chiwinga
Hamna Ibara yoyote ile  katika katiba ya  Tanzania inayomlazimisha Rais we Tanzani kuteua wabunge kwa uwiano wa  kijinsia.
Naona kuna baadhi ya watu wanapiga chapuo huenda kuteuliwa kw Daktari wa sheria Abdallah Possi  (pichani) kuwa Balozi huenda kumesababishwa na hatua ya Rais Magufuli kuteua wabunge sita wa kiume na wawili wa kike na kwamba anavunja ibara ya 66(e). 
Kwanza ieleweke kwa mujibu wa sharia katiba inayotumika na  kutambulika ni ile iliyochapishwa katika lugha ya kiswahili ambayo haijaweka masharti kwa Rais kuteua wabunge kwa uwiano wa kijinsia.
Kwa mujibu wa kifungu cha  84 ya Interpretation of Laws Act 
(1)Lugha za sheria za Tanzania zitakuwa ni Kiswahili au Kiingereza au lugha zote mbili.
(2) Pale ambapo Sheria yoyote imetafsiriwa kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine na kuchapishwa kwa lugha zote mbili, na iwapo itatokea mgongano au kutakuwa na mashaka ya maana ya maneno, maelezo, lugha ambayo imetumika wakati wa kupitisha Sheria hiyo na Bunge ndiyo itakayokuwa ya kipaumbele.
Kifungu kilichonakiliwa hapo juu kinaelekeza kwamba iwapo sheria imechapishwa kwa lugha zote mbili na ikatokea mgongano au mashaka katika maneno/ maelezo yaani  toleo la lugha moja linakuwa na maana inayokinzana/tofautiana na toleo la lugha nyingine, kinachotakiwa kutumika hapa ni toleo la lugha ambayo ilitumika na Bunge kuipitisha sheria husika. 
Swali muhimu sana je lugha ipi basi amabayo ilitumika kuipitisha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania??? Katika kesi Daudi Pete v. Republic [1993] TLR 22 at p. 33  mahakama iliweka bayana kwamba; "that the controlling version of the Constitution is the Kiswahili one and not the English version because the Constitution was enacted in Kiswahili." (Maana yake ni kwamba toleo la kiswahili la Katiba ndiyo lenye nguvu na sio toleo la Kiingereza kwa sababu Katiba ilipitishwa katika lugha ya Kiswahili.) 
Kwa hiyo basi kutokana na uamuzi wa Mahakama katika kesi ya Daudi Pete pale inapotokea kuna tofauti ya maana au maelezo baina ya toleo la Kiswahili la Katiba na toleo la Kiingereza la Katiba, maana iliyopo kwenye toleo la Kiswahili ndiyo itakayotumika. 
Kwa maelezo hayo niliyotoa ni dhahiri kuwa uamuzi wa Rais Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuteua  wabunge wengi wa kiume uko sahihi kisheria wala hajavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Dr Possi ameteuliwa kua Balozi ni kutokana na sifa  kielimu  ,weledi wake uzoefu, uadilifu wake na uchapakazi wake na sio kwa lengo la "kubalance" uwiano wa kijinsia kama baadhi ya watu wanavyopotosha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...