Na Zuena Msuya, Iringa

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini, Unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Awamu ya kwanza na ya Pili ili kuona thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika mradi huo.

Mwenyekiti wa PAC, Livingstone Lusinde alisema hayo mkoani Iringa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA, katika vijiji na Taasisi mbalimbali zilizopitiwa na Mradi huo.

Lusinde alifafanua kuwa wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo baada ya kuona miundombinu iliyotumika na maendeleo ya wananchi katika maeneo ambayo yamepitiwa na miradi hiyo.

” Tumepita katika vijiji mbalimbali hapa Iringa ambayo nimepitiwa na REA,tumeona namna ambavyo mradi huo umetekelezwa na tumeona miundombinu iliyotumika na maendeleo yake hivyo hatuna budi kusema wazi kuwa tumeridhishwa na utekelezaji wa mradi huu”, Alisema Lusinde.

Lusinde aliwasisitiza wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Umeme vijijini, kutumia miundombinu imara inayokwenda sambamba na thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika kutekeleza wa miradi hiyo ili kutimiza malengo yaliokusudiwa na kuondoa hasara za makusudi zinazoweza kujitokeza.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Livingstone Lusinde( kulia) wasikiliza hoja za Wajumbe wa Kamati ya PAC, (hawapo pichani) kabla ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini mkoani Iringa.
Wajumbe wa Kamati ya PAC, wakisikiliza taarifa ya Mkoa wa Iringa, kabla ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa MIRADI ya Umeme vijijini mkoani Iringa.
Wajumbe wa Kamati ya PAC,wakikagua Miradi ya Umeme Vijijini katika kijiji cha Nyamahana mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Livingstone Lusinde ( kushoto) akiruka pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Umeme Vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...