Picha za awali za wahusika wa waraka huu ikiwa ni pamoja na watoto Amina na Seleman Kichawela na Bw. Mahmud Hassan Mihile aliyewachukua miaka 22 iliyopita ili kuwasaidia masomo huko Uingereza.

Kutokana na kichwa cha habari hapo juu mimi AZAMA ABBASI KICHAWELE ambae kwa sasa ni mjane, mwenye namba ya simu +255 784 697319 na mkazi wa Majengo Arusha, Tanzania, na ambae ni mama wa nyumbani, nachukua nafasi hii kukutaarifu kama ifuatavyo.
Mume wangu kwa majina ABBASI ALLY KICHAWELE ambaye kwa sasa ni marehemu alikua na rafiki wake wa karibu kwa majina MAHMUD HASSAN MIHILE aliekuwa akitumia namba ya simu +441332270462 wakati huo mwenye asili ya Kisomali na uraia wa Uingereza na Tanzania walikubaliana awachukue watoto wetu ambao ni: SELEMAN ABBASI KICHAWELE aliekuwa na umri wa miaka kumi na AMINA JABIRI KICHAWELE aliekuwa na umri wa miaka saba aende nao Uingereza kwa ajili ya kuwasomesha.
Siku ya kuondoka watoto hawa ilikuwa ni mwaka 1994 na waliondoka na mke wa huyo Msomali kwa majina RAHMA MIHILE.
Mji wa kwanza walioshukia huko UINGEREZA unaitwa LEICESTER.
Baada ya hapo mawasiliano yaliendelea kuwepo kati ya mzazi wa kiume wa watoto na Msomali.
NB: Katika hawa watoto huyu wa kike, Amina Jabiri alikuwa ni wa mdogo wake mume wangu yaani shemeji yangu.
Kwa bahati mbaya mume wangu, aliugua maradhi ya cancer na ilipofika mwaka 1998, nikampoteza (alitangulia mbele ya haki)
Baada ya kifo cha mume wangu hakukua na mawasiliano yoyote kati yangu na huyu bwana aliyechukua watoto wangu. Alikata mawasiliano kabisa na wala hakutaka watoto wajue kuwa baba yao hayupo tena Duniani.
Kwa bahati mbaya sikua na mtu mwingine mbadala wa kuweza kuniunganisha na huyu bwana ikizingatiwa pia mimi ni mama wa nyumbani sikuwa na PR kubwa.
Leo hii ninapoandika barua hii, huu ni mwaka wa ishirini na mbili (22) toka nitengane na watoto wangu. Sisi pamoja na wanafamilia tutaendelea kutoa shukrani zetu kwa serikali ya Uingereza iwapo watoto hawa wapo salama na kwenye ajira zao. Kwetu hilo sio tatizo.
Jambo kubwa linaloniumiza ni kutokua na MAWASILIANO na watoto wangu kwa miaka ishirini na mbili sasa. Wakati mwingine najenga wasiwasi kwamba je, wako hai? Na hali hii nitaendelea nayo mpaka lini? 
Huyu bwana Mahamudu (msomali) nini kimemsukuma kuwa na ujasiri wa kuwaficha watoto wangu hata nisiwe na mawasiliano nao? Ana dhamira gain?
Kutokana na maelezo mafupi hapo juu nimefikia hatua ya kuiomba ofisi yako tukufu kunisaidia kupata namna ya kuwasiliana na watoto wangu wapendwa huko waliko. Jambo hili likifanikiwa litaleta faraja sana kwangu na kwa wana familia kwa ujumla.
Pia itakuwa ni fursa kwa watoto kutambua kuwa baba yao mpendwa alishafariki lakini mimi mama yao bado nipo hai, taarifa ambazo tuna hakika hawajazipata. Naambatanisha picha za watoto ambazo walipigwa wakati wanakaribia kuondoka mwaka 1994.
Pia naambatinisha na picha ya Mahmud Hassan Mihile (Msomali) ya wakati huo aliyewachukua watoto kwa makubaliano na mume wangu.

NB: Kwa mawasiliano tumia namba hizi za barua pepe
Au Athuman Rashid Mfinanga
Box 2614, - Arusha Tanzania
Ph: 0754375602/0784375602
 
Wako,
Katika ujenzi wa Taifa
Azama Abbasi Kichawele

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. dada yangu umechelewa sana kutafuta msaada, miaka 22 ni mingi na hao si watoto tena ni watu wazima. kwa tabia za ulaya ukifika miaka 18 unajitegemea , sidhani kama bado wapo kwenye himaya ya aliyo wachukua,lakini usikate tamaa tafuta mawasiliano utapata mji wa leicester wapo wabongo na wa zenj wengi tu pengine kuna anae wajua
    kila la kheri

    ReplyDelete
  2. Huyo mdau aliosema Umechelewa asikukatishe Tamaa hata kidogo.

    Mimi binafsi nilipoteza kaka yangu for 35 yrs Kwa uwezo wake Mungu mkarimu tumempata sehemu Hatukutegemea. Mzima wa Afya na Mpk leo Alhamdulillah tuko pamoja.

    Mama unaehusika na Issue hii HUJACHELEWA HATA KIDOGO.

    Ninachokushauri tafuta Mbunge wako akupe Barua ya utambulisho kuhusu kesi yako hii Kisha Mwambie aandike Barua ya kukutambulisha inayoelezea Kesi yako kisha Nenda Nayo UBALOZI WA UINGEREZA HAPO DARESALAAM toa vielelezo vyote na Majina kamili na tarehe zao za Kuzaliwa. Ukipata majibu Yalete hapa tuendelee Kufuatilia.

    Ktk Hizo namba ulizoweka hapo Juu Inaonekana Hazifanyi kazi lkn Hapa Uingereza Kumpata aliyekuwa na Namba hizo Sio Kazi kubwa sana hata km ALISHAHAMA hapo . Na namba Hizo zina link na Miji miwili;, Derby na Leicester.
    Na Jumuia ya Wanao ongea Kiswahili Ktk Miji hio Zinajulikana na Sio Kubwa sana.

    Kuna uwezekano mkubwa hawa wanao walipewa malezi ya kuambiwa wao hawana Wazazi au wao ni yatima na Ndio maana wakawa Kimya mpk sasa.
    lkn HUU NI MWANZO MZURI. usikate tamaa hata siku Moja. Na Mungu akipenda km wanao wako Hai Utawapata.

    Habari Hii nashauri Yyt aliyeguswa Aisambaze Ktk Kila chombo cha habari anachoweza kukipata. Ikiwemo IPP Media, Jamii Forum and so on

    Tuko pamoja Mama Muhusika na Mungu yuko na Wewe na mimi Niko na Wewe .
    Na Watanzania wote walioko Huku Uingereza nina imani Watafanya chochote Kukusaidia kuwapata Wanao.

    Kesi Km Hizi ni NYINGI MNO na Mara zote zinakuwa na MWISHO MWEMA wala.Usidhani Uko Peke yako.


    Mimi ndugu yako
    Abu Fahmi.
    United Kingdom.

    ReplyDelete
  3. Kaka Abu Fahmi huweizi kumsaidia uyu mama kumtolea tangazo kwenye gazeti lolote la bule apo United K.
    nafikili utakuwa msaada mkubwa facebook? kwa kutumia majina yao?

    Asante sana

    ReplyDelete
  4. Narudia tena hawa si watoto tena ni watu wazima pengine tayari wanafamilia zao.hao kusema ufungue kesi ubalozini ukusaidie sidhani.wanaweza kupatikana na wakakataa mawasiliano na hakuna wakuwalazimisha ni hiari yao.wapo huru kukubali mawasiliano au kukataa .lakini tusiombe hivyo.tuwasaidie tu kuwatafuta wakipatikana tuwape namba za wazazi wao. Lakini kuenda ubalozini na detail zao is too late.wengekua bado wadogo chini ya miaka 18 ingekua na nguvu.

    ReplyDelete
  5. Kwa taarifa za awali hawa wanaotafutwa walikabidhiwa social care walipo kua bado ni watoto.hawakuelewana kimalezi na huyo aliye wachukua. Ndugu yangu fahmi kama upo karibu na mji wa leicester jaribu kuulizia social care ya hapo pengine utapata mwangaza wapo wapi kwa sasa .itabidi ujieleze vizuri si unajua mambo ya europe hiyo ni private issue
    All the best

    ReplyDelete
  6. JAMANI MIMI NI GRACE NAISHI HOLLAND. ASANTENI SANA WATOTO WAMEPATIKANA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari dada, leo hii 23 February 2022 niko ofisi moja na mama yake mzazi AMINA na anasema bado hajapata bahati ya kuwasiliana na mwanaye. Hakika mzazi huyu anapitia magumu sana bila kuwasiliana na mtoto wake wa kumzaa na huku akisikia kuwa yuko hai nje ya nchi, nadhani akimsikia tu atapata faraja kubwa sana. Asante.

      Delete
  7. JAMANI MIMI NI GRACE NAISHI HOLLAND. ASANTENI SANA WATOTO WAMEPATIKANA.

    ReplyDelete
  8. JAMANI MIMI NI GRACE NAISHI HOLLAND. ASANTENI SANA WATOTO WAMEPATIKANA.

    ReplyDelete
  9. Ndugu Hijambi na wadau wengine habari nilizopata mpk sasa watoto wamepatikana wakiwa wazima na afya njema.

    Tumshukuru Mungu mkarimu kwa kuliwezesha hili Zoezi.

    Alhamdulillah Rabb l aalamiin.

    Mbarikiwe sana wote mlioshiriki ktk Zoezi hili.
    Na km kuna Mzazi au wazazi wengine out there waliopoteza watoto wao walete habari zao hapa tuone namna gani tunaweza kusaidiana. Wasikate tamaa hata kidogo.
    Ukimtegemea Mungu Hakuna kinachoshindikana.

    Ndugu yenu Abu Fahmi.
    United Kingdom.

    ReplyDelete
  10. Assalam alykum ya Abu Fahmi.

    Alhamdulillah na allah azidi wabariki kwa jitihada zenu za dhati.
    Lakini ukweli nikwamba nimekutana na mzazi mmoja wa huyo mtoto wa kike (Amina Jaabir Kichawele), na anadai bado wanawatauta watoto wao, hawajawapata mpaka leo hii japo wanasikia watoto wapo hai na salaama.. hata sasa ninapoandika comment hii nipo na huyu mama..

    OMBI LANGU KWENU WADAU:

    KAMA KUNA YOYOTE MWENYE MAWASILIANO YA HAO VIJANA KWANI SIO WATOTO TENA, ATUTUMIE ILI WAZAZI WAO WAWEZE WASILIANA NAO. HATA KAMA NI ACCOUNT ZAO ZA FACEBOOK,WHATSAPP,TWITER,INSTAGRAM AMA YOYOTE ILE.

    TAFADHALI TUWASILIANE :

    EMAIL : thelostchildrentz@gmail.com
    PHONE : +255 718 945 698
    Shukrani za dhati kwa wote waliojitolea kuwasaidia wazazi hawa
    Ndugu yenu Daffy S. Mwarabu

    ReplyDelete
    Replies
    1. A'salaam Alaykum akhiy... hii February 2022 niko na huyo mama ofisi moja Arusha, bado anamtafuta mwanaye, nadhani wamepatikana ila either hawajaamua au hawajapewa nafasi ya kuwasiliana.

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...