Na Ofisa habari Mufindi.

Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh. Angelina Mabula, amesema serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa dhati kupunguza kwa asilimia kubwa kama si kuondosha kabisa kero ya migogoro ya ardhi nchini ili kuondokana malumbano yanayozikabili jamii nyingi hapa nchini.

Mh. Mabula ameyasema hayo mjini Mafinga wakati wa ziara ya kikazi aliyofanya Wilayani Mufindi akiwa na lengo la kukagua masuala mbalimbali yaliyo chini ya wizara yake sanjari na kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na migogoro ya ardhi.

Amesema kwa muda mrefu jamii nyingi hapa nchini zimekuwa katika migogoro ya kugombea ardhi, jambo ambalo linachochea mafarakano miongoni mwa wananchi hivyo serikali ya awamu ya tano imejidhatiti kuhakikisha inapunguza au kuondosha kabisa migogoro iliyopo na akatoa rai kwa wakurugenzi wa halmshauri kuhakikisha wanasimamia vema masuala ya ardhi ili kuzuia kuibuka kwa migogoro mipya.

Aidha, amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Mji wa Mafinga kuhakikisha anarasimisha makazi ya wakazi wa kata ya Kinyanambo iliyopo mjini Mafinga kwa kuhakikisha kuwa makazi yao yanapimwa na wanapatiwa hati ili wamiliki maeneo yao kisheria jambo ambalo litawafanya waishi kwa kujiamini katika maeneo yao lakini pia waweze kuzitumia hati hizo kama dhamana katika taasisi za kifedha.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiongea na wananchi katika ukumbi wa CCM mjini Mafinga kabla hajaanza kusikiliza kero zao.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa wamiliki wa ardhi alipotembelea ofisi za ardhi Wilayani Mufindi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William mara baada ya kukagua mfumo unaohifadhi takwimu za wamiliki wa ardhi Wilayani Mufindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...