Na Bashir Yakub.
Hivi karibuni kumeibuka miradi mingi binafsi na ya serikali hasa kupitia NHC ya ujenzi wa nyumba za pamoja. Miradi ipo kwa majina tofauti ipo inayoitwa APARTMENT, CITY, VILLAGE, TOWN, n.k. Baadhi ipo kigamboni, Arusha na maeneo mengine .
Pia ipo katika mitindo tofauti ipo ile ya maghorofa ya kwenda juu, maghorofa ya mshazali, na ile ya nyumba moja moja lakini katika eneo moja (common ground).
Kutokana na hilo makala yalenga kukufahamisha usinunue tu kwa kupenda muonekano,mazingira na rangi , bali pia uwe na uhakika wa faraja(comfortability) inayotokana na mambo mengine nje ya muonekano, rangi na mazingira.
1.TOFAUTI KATI YA NYUMBA ZA MIRADI NA NYUMBA ZA KAWAIDA.
Ipo tofauti kati ya nyumba za kawaida tulizozoea na hizi za miradi zilizotajwa humu. Tofauti ipo katika ngeli hizi :
( a ) Taratibu zake za ununuzi.
( b ) Vitu unavotakiwa kujua kabla ya ununuzi.
( c ) Sheria zinazozilinda na,
( d ) Maisha yako baada ya kuwa umenununua.
Makala yataeleza vitu unavyotakiwa kujua vinavyotofautisha nyumba hizi na nyingine za kawaida.
2. VITU UNAVYOTAKIWA KUJUA.
( a ) Uwepo wa malipo na michango mbalimbali. Pamoja na kuwa ni mali yako umenunua , kanuni ya 15( 2 ) ya The Unit Title Regulations, G.N 357/2009 imeeleza baadhi ya michango. Ipo michango kwa ajili ya chama na uongozi, michango kwa ajili ya maeneo ya matumizi ya pamoja, michango kwa ajili ya huduma mbalimbali mnazotumia pamoja.
Michango hapa haihusishi bili zako za umeme,maji n.k. Michango hii inaweza kuwa inalipwa kila mwezi au vinginevyo kadri ya utaratibu wa eneo husika.
Hii ni tofauti na nyumba za kawaida ambazo haziko katika mfumo huu ambapo ukinunua umenunua hakuna mchango wa chama au vinginevyo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...