Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia masuala ya Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajia kushiriki uzinduzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka tukio linalotarajiwa kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jijini Dar es salama kesho asubuhi.

Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia,  amelakiwa na Mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo anayehudumu katika Nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi, Bibi Bella Bird.

Akiwa nchini, Bw. Diop atakutana na kufanya mazungumzo pia Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango,  Gavana wa Benki Kuu Benno Ndulu, Sekta Binafsi ambapo mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita katika Miradi kadhaa ya maendeleo inayofadhiliwa ama kugharamiwa na Benki hiyo kwa njia ya ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu ambayo mpaka sasa inakadiriwa kufikia thamani ya Dola Bilioni 4 nukta 7 .
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa na Mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, wakiwa katika chumba cha kupumzikia wageni maalumu katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bi. Bella Bird.
 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (wa pili kushoto aliyeshika dafu) alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) ambapo anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017, na baadaye kufanya mazungunzo na Waziri huyo alasiri.
 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (kushoto) akinywa maji ya dafu  alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) ambapo anatarajiwa kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi, baada ya mapokezi ya Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...