Muwakilishi wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi nchini (TPBC), Joe Anae (kati) akiwatambulisha Mabondia Ramadhan Shauri (kulia) na Meshark Mwankemwa (kushoto) watakaozichapa Februari 5, 2017 katika uwanja wa ndani wa Taifa, Jijini Dar es salaam ikiwa ni mpambano wa kuwania mkanda wa Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (66.7kg  Welterweight). ulioandaliwa na Promota wa mchezo wa ngumi "Masumbwi" wa muda mrefu, Sadick Kinyogoli kupitia Kampuni yake ya SADICK  & CO. LTD, Mambondia hao wametambiana kwa kila mmoja kuonyesha nia ya kumshinda mwenzake katika mpambano huo. Kabla ya pambano la Mabondia Ramadhan Shauri na Meshark Mwankemwa, kutakuwa na mapambano ya utangulizi yapatayo saba, likiwepo lile lililosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mchezo wa masumbwi la Mabondia Mohamed Matumla  na Mfaume Mfaume (62 KG  LIGHT weight).
 Muwakilishi wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi nchini (TPBC), Joe Anae (wa pili kulia) akimkabidhi fedha Bondia Meshark Mwankemwa kwa maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Bondia Ramadhan Shauri (kulia).
 Muwakilishi wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi nchini (TPBC), Joe Anae (katikati) akimkabidhi fedha Bondia Ramadhan Shauri kwa maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Bondia Meshark Mwankemwa.
 Bondia Ramadhan Shauri akimwaga wino kukubali kuzichapa na Bondia Meshark Mwankemwa
 Naye Bondia Meshark Mwankemwa akimwaga wino kukubali kukipiga na Bondia Ramadhan Shauri.
Muwakilishi wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi nchini (TPBC), Joe Anae akiwatambulisha Mabondia Mohamed Matumla (kulia) na Mfaume Mfaume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...