Na Woinde Shizza,Arusha

Mfanya biashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Moshi (30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.

Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya .

Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa mahakamani.

Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo. Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri unatarajia kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha .Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa february 6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.

Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho. Alisema ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...