Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi Morogoro.

Jeshi la Polisi nchini, limeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD) ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama wao kote nchini huku ikiweka dhamira ya kutoza riba ya mkopo kwa  asilimia 10.5 kwa mwaka.

Akifungua mafunzo ya siku mbili yanayofanyika mkoani Morogoro, Kaimu kamanda wa Polisi hapa (ACP) Leonce Rwegasila, alisema kuwa, kwa kuzingatia umuhimu na uzito wa mkutano huu ni vyema kila mshiriki akazingatia mahudhui ya kile kitakachotolewa ili kuwa mjumbe mzuri kwa kupeleka elimu mahala alikotoka, alisema.

Hata hivyo, alisema, katika mafunzo haya zipo mada pamoja na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa ili kuja na majibu mujarabu yatakayowezesha kuwa na Saccos imara na yenye kukidhi mahitaji kwa  wanachama wao ambao ni askari Polisi pamoja na familia zao.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa URA SACCOS LTD (SSP) Kim O. Mwemfula, alisema zipo huduma zilizoanzishwa za uhakika za ushirika wa kuweka akiba na kukopa kupitia Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), ambapo askari aliye mwanachama wa ushirika huo uweza kuweka na kukopa kwa riba nafuu ili kuweza kuboresha maisha yake na familia yake katika Nyanja za Kielimu, Biashara na hata Ujenzi wa nyumba.

Ameongeza kuwa, masuala ya ustawi kwa askari yamesaidia kujenga utulivu wa akili kwa askari Polisi pamoja na kuboresha suala la ustawi wa usalama wa raia na mali zao na kulifanya taifa kuwa la amani na utulivu na kukabiliana na aina zote za matishio ya kiuhalifu na wahalifu.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akipokea taarifa ya washiriki wa mkutano mkuu wa nane wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), kutoka kwa (ASP) Emmanuel Katabi, kulia ni Meneja Mkuu wa URA SACCOS (SSP) Kim O. Mwemfula, na wamwisho ni (ASP) Bakari H. Mzungu.
Mwezeshaji Mkaguzi wa Polisi (INSP) Edwin B. Mkole , akiwasilisha mada kuhusiana na taratibu za utoaji wa mikopo kwa wanachama wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakati wa mkutano mkuu wa nane wa chama hicho unaofanyika mkoani Morogoro.

Baadhi ya watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakiwasili mkoani Morogoro, kuhudhuria mkutano mkuu wa nane wa chama hicho utakaofanyia kwa muda wa siku mbili na kuwashirikisha watendaji na wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

    Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa nane unaofanyika mkoani Morogoro. (Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...