Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan akiwa ameambana na mkewe Mama Emine Erdogan, wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Erdogan atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia leo tarehe 22 Januari, 2017. 
 RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na mgeni wake
 RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan mara baada ya kuwasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,kulia ni mke wa Rais wa Uturuki,Mama Emine Erdogan

RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak. Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...