Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.

VIKUNDI 40 vyenye wasanii 400 vinatarajiwa kutumbuiza Tamasha la Sauti za Busara linalotarajia kuanza kuridima Februari 9 -12 katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Mjini Zanzibar .

Akizungmza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Sauti za Busara, Simai Said amesema kuwa tamasha limekuwa likitangaza Tanzania pamoja na kuwaweka Waafrika sehemu moja.

Simai ameiomba Serikali kuunga mkono Sauti za Busara kutokana na kazi kubwa inayofanyika katika kuongezea uchumi wa nchi pamoja na kupata watalii wengi wakati tamasha hilo linapofanyika. Amesema kutokana na Tamasha hilo kuwa na vitu vingi vya kiubunifu imesaidia kuongeza ajira kwa vijana katika pande zote kutokana na kuutumia utamaduni wa Tanzania.

“Sauti za Busara limebakiza siku chache kufanyika pale Mji Mkongwe, Zanzibar 9-12/Februari kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa tamasha la Sauti za Busara lenye kauli mbiu ya ‘AfricaUnited’ mwaka huu tamasha litakua na majukwaa matatu yatakayotumiwa na wasanii wote kimataifa/nyumbani”amesema Simai.
Mwenyekiti wa Bodi wa Sauti za Busara,Simai Said akitoa ufafanuzi na namna tamasha hilo litakavyokuwa siku hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani),ambapo ameeleza kuwa tamasha hilo ambalo limekuwa likiwajumuisha makundi,washabiki na wapenzi mbalimbali litabeba kauli mbiu itakayojulikana #AfricaUnited.Kulia ni ni Balozi Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne – Marie Kaarstad .

Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne – Marie Kaarstad (pichani kulia) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusiana na udhamini wao katika tamasha la Sauti za Busara linalotarajiwa kuanza kurindima Februari 9-12 mjini Ngome Kongwe,Zanzibar,Balozi huyo pia amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kulidhamini tamasha hilo ambalo limekua likiibua vipaji mbalimbali na kivitangaza nchini na ulimwengu kwa ujumla,Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Sauti za Busara,Simai Said,Mkurugenzi wa tamasha hilo Yusuph Mahmoud pamoja na Meneja wa tamasha hilo,Journey Ramadhan.
Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara,Yusuph Mahmoud akielezea mambo mbalimbali yatakayojiri ndani ya tamasha hilo,Simai alieleza kuwa tamasha hilo Wasanii watatumbuiza LIVE kwa asilimia 100.
Viongozi wa tamasha la Sauti za Busara wakizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar. PICHA NA MICHUZI JR.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...