Dotto Mwaibale, Dodoma

SERIKALI imesema itaangalia upya taratibu na kanuni zilizopo ili kuharakisha tafiti za kilimo zinazofanyika nchini zianzekufanya kazi kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo asubuhi.

"Binafsi nisema katika teknolojia hii ya uhandisi jeni kwa hapa nchini tumechelewa kutokana na taratibu na kanuni zetu kutuchelewesha kwani maarifa ya watafiti wetu hayawafii walengwa kutokana na kanunu hizo" alisema Tizeba.Alisema ni lazima serikali kuangalia jambo hilo ili kufupisha matokeo ya utafiti wa wataalamu wetu kuendelea kufanya hivyo ni kucheleweshana.

Alisema mbegu hii ambayo inafanyiwa utafiti kwa wenzetu wa Afrika Kusini wameanza kuitumia wakulima wao lakini kwa sisi kwa utaratibu wetu mbegu hiyo tutaanza kuitumia mwaka 2021 ni miaka minne zaidi.

"Tusisubiri taratibu hizi tutazungumza na wenzetu wa Ofisi ya Mkamu wa Rais  Mazingira na Tume ya Taifa Sayansi na Teknlojia (Costech) ili kuona namna ya kupunguza taratibu na kanuni hizo ambazo hazina tija kwa mkulima.

Alisema kama utafiti umefanyika na ukatoa matokeo mazuri hakuna sababu ya kusubiri na kupoteza muda wa matumizi ya teknolojia hiyo.Alisema leo tabia nchi imeendelea kukua na ukame lakini sisi tunajifunga katika jambo ili ni lazima tujipange na kutumia teknolojia hii muhimu.
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kushoto), akizungumza na watafiti wa kilimo na wanahabari (hawapo pichani), wakati alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda.
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso.
 Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Tizeba.
 Taswira ya shamba hilo la jaribio la mbegu za mahindi lililopo Makutupora mkoani Dodoma.
Waziri Tizeba  (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo baada ya kutembelea shamba hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...