JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU


1.         Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inatekeleza Programu ya Kukuza Stadi za Kazi Nchini ya miaka mitano (2016 -2021) ambayo imelenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Hivyo, OWM-KVAU imeingia makubaliano na

Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam Kampasi ya Mwanza iliyo eneo la Ilemela Mwanza, kutoa mafunzo ya stadi za kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi. Lengo ni kuhakikisha nchi inakua na nguvu kazi ya kutosha yenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira katika kutengeneza bidhaa za ngozi nchini.

2.         Ofisi inapenda kutangaza nafasi 1,000 za mafunzo yatakayoanza ifikapo tarehe 20 Februari, 2017 katika Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam Kampasi ya Mwanza. Vijana wa Kitanzania, wenye elimu ya msingi na kuendelea na umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo wawasilishe maombi yao kuanzia tarehe 22/ 01/2017 hadi 04/02/2017 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:

(i)      Barua ya maombi yenye anuani kamili ikiwa na namba za simu pamoja na barua pepe;

(ii)      Nakala ya Cheti cha Elimu uliyohitimu
(iii)       Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kadi ya mpiga kura;
(iv)      Barua  ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa anaoishi mwombaji; na
(v)      Picha nne za paspoti.

3.         Maombi yawasilishwe kwa Mkuu wa Kampasi, TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM – KAMPASI YA MWANZA, S.L.P. 2525, Mwanza au kwa barua pepe: info@mwanzacampus.dit.ac.tz

4.         Watakao kuwa na sifa na vigezo wataitwa kwenye usaili kuanzia tarehe 8 hadi 11 Februari, 2017.


IMETOLEWA NA:
KATIBU MKUU
18 Januari, 2017

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...