Na. Aron Msigwa – NEC,
Zanzibar.
Hatimaye wananchi wa
Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Mpiga leo wamejitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali kupiga kura kumchagua
Mbunge atakayewawakilisha kwa kipindi cha miaka miaka 4.
Zoezi la upigaji wa
Kura katika vituo mbalimbali lilianza majira ya saa 1 asubuhi likifanyika kwa hali ya Amani na Utulivu huku
baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakipongeza maandalizi mazuri
yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzine (NEC) kufanikisha Uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza kuhusu
mwenendo wa Uchaguzi huo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo hilo na kuzungumza na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo
vituoni, Waangalizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi huo amesema Tume imeridhishwa na kazi nzuri iliyokuwa ikiendelea katika vituo mbalimbali
vya kupigia Kura.
“ Viongozi wa Tume tumetembelea
vituo mbalimbali vya kupigia Kura katika jimbo la Dimani; tumeona wenyewe
upigaji wa Kura unaendelea vizuri, tumewauliza Mawakala, Watazamaji na Wasimamizi
wa Vituo vya Uchaguzi kila mmoja amesema
Uchaguzi unakwenda vizuri, nachoweza kuwaambia watanzania Uchaguzi Dimani
unakwenda Vizuri” Amesema Jaji Kaijage.
Amesema Wasimamizi wa
Uchaguzi katika Jimbo hilo wanaendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria,
Kanuni na Maadili pia kushughulikia kwa haraka changamoto zilizokuwa
zikijitokeza katika baadhi ya vituo vya
kupigia Kura.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na Msimamizi kituo cha Dimani Bi. Abdu Simai Haji leo wakati zoezi la upigaji kura likiendelea katika jimbo la Dimani.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa Zanzibar kutoa tathmini ya hali ya Uchaguzi mara baada ya kuetembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura katika jimbo la Dimani leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (wa pili ) akiwa ameambatana na Baadhi ya Watendaji wa NEC na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Bi. Idaya Selemani Hamza (wa Kwanza) akiwasili katika kituo cha Kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani kuangalia maendeleo ya Upigaji wa Kura leo.
Mmoja wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika jimbo la Dimani leo.
Baadhi ya Wangalizi wa Uchaguzi katika jimbo la Dimani wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...