Na. Aron Msigwa –NEC, Zanzibar.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wananchi wanaoishi katika kata 19 zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Madiwani kwa upande Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Zanzibar, Januari 22, 2017 wajitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka 3.

Akizungumza na vyombo vya Habari leo mjini Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles kaijage amesema kuwa maadalizi ya Uchaguzi huo yamekamilika na wananchi wote wenye sifa za kupiga kura katika uchaguzi wajitokeze wingi kutimiza wajibu wao wa Kikatiba.

Mhe. Kaijage amewapongeza wananchi wanaoishi katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na wale wa Kata 19 za Tanzania Bara watakaofanya uchaguzi mdogo hapo kesho (Januari 22, 2017) kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha Kampeni za wagombea wa vyama mbalimbali vya Siasa.

Amesema licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale zilizojitokeza zikiwemo za ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwa baadhi ya Vyama na wagombea wao, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilichukua hatua za kukemea vitendo hivyo ili kuwezesha Kampeni za Uchaguzi kufanyika kwa Usalama na Amani.

“Licha ya kwamba kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika vituo vya kupigia kura, Ni matumaini ya Tume kuwa hali ya Amani na Utulivu ambayo imekuwepo hadi sasa na kama ilivyokuwa katika Chaguzi zilizopita itaendelea kudumishwa ili kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa Utulivu, Amani na Ustawi wa Taifa letu” Amesema Jaji Kaijage.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akitoa Risala kuhusu upigaji wa Kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na Kata 19 za Tanzania Bara leo mjini Zanzibar. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Kisheria ya kuzingatiwa na wapiga Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika kesho, Januari 22, 2017. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage.
Waandishi wa Habari wakiuliza maswali mbalimbali wakati wa Mkutano huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...