Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
ametoa agizo kwa viongozi wote nchini kuacha mara moja kuwakamata
wauguzi, wakunga na kuwaweka ndani na badala yake wanapaswa kufuata
taratibu zilizopo.
Akizungumza
hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Mkunga Okoa Maisha Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema
wakunga wanalo baraza ambako ndilo suluhishi la matatizo yao.
"Aidha
Mhe. Ummy amesema kuwa pale ambapo muuguzi au mkunga anapokosea zipo
taratibu za kufuata na siyo kumweka ndani kwani kuna Baraza la Wakunga
ambalo lina Mamlaka ya kisheria za kuchukua kwa mkunga yoyote ambaye
amekwenda kinyume.
"Tunao
Wakunga na wauguzi ambao wanafanya kazi zaidi ya masaa, tumeona
kilichotokea Sikonge, kiongozi anakuja juu kwanini mtoto amepewa dawa ya
Quinn," alisema Ummy.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda
Leshabari amesema kuwa mradi huo unalenga kupunguza vifo katika Mikoa
ya Shinyanga na Simiyu hivyo wauguzi na wakunga ni vema wakashirikiana
na Baraza hilo ili kufanikisha malengo yao.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na wadau wa Baraza la Baraza la Wakunga hawapo pichani wakati wa kuzindua mradi wa Mkunga Okoa Maisha kwa kushirikiana na watu wa Canada.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kuzindua mradi wa Mkunga Okoa Maisha , wa kwanza kushoto ni Balozi wa Canada Bi. Susan Steffan na wakawnza kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...