Kikosi cha Yanga

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mabingwa watetezi wa kombe la Shirikisho FA Yanga wanatarajiwa kushuka dimbani leo kupambana na wauza mitumba wa Ilala Ashanti  United katika mchezo wa hatua ya 32 ya kombe hilo ikiwa ni raundi ya Tano toka kuanza kwa msimu wa pili wa mashindano hayo.
Kikosi hicho cha Mzambia George Lwandamina, kikiwa kimetoka kupata ushindi wa ugenini dhidi ya Majimaji ya Songea watashuka  katika Uwanja wa Uhuru kuhakikisha wanaendeleza kutetea ubingwa wao huku wakiwakosa nyota wao kadhaa.
Akizungumza na globu hii, Kocha msaidizi Juma Mwambusi amesema kuwa kikosi chake kimejianda kikamilifu kwa ajili ya kutoka na ushindi na wana matumaini  na vijana wao kwani   watajituma kulingana na maelezo waliyowafundisha ili kutetea kombe hilo.
"wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri huku wakiwa na morali ya kushinda ili kujiweka kwenye mazingira  mazuri katika michuano na kuendelea kulitetea kombe letu hata hivyo katika mchezo wa kesho tutawakosa nyota wetu kadhaa ambao bado ni majeruhi lakini Donald Ngoma hatakuwepo kwakuwa amefiwa na kaka yake na amesafiri kwenda nchini Zimbabwe, "amesema Mwambusi.
Wachezaji watakaowakosa katika mchezo huo ni  Donald Ngoma,Obbey Chirwa, Justin Zullu na ,Vicent Bossou anayeitumika timu yake ya Taifa ya Togo.
Emauel Martin na Malimi Busungu wameungana na wachezaji wenzao kwenye mazoeezi ya leo kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Ashanti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...