Mheshimiwa Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa akiwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa François Hollande, Rais wa Jamhuri ya Ufaransa leo tarehe 23 Februari, 2017, Ikulu ya Ufaransa. Katikati ni Mheshimiwa Jean Marc Ayrault, Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa wa Ufaransa
 Mheshimiwa Balozi Shelukindo akiwa kwenye mazungumzo rasmi na Mheshimiwa Rais François Hollande baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho.
Mheshimiwa Balozi Shelukindo na Mheshimiwa Hollande wakiendelea na mazungumzo kwenye Ikulu ya Ufaransa. Kulia kwa Mheshimiwa Hollande ni Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa ya Ufaransa, Mheshimiwa Jean-Marc Ayrault na kulia kwa Balozi Shelukindo ni Bwana Stephen Wambura, Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Kaimu Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania mjini Paris.
Mhe. Balozi Shelukindo akiagana na Mhe. Rais Hollande wa Ufaransa, baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwenye Ikulu ya nchi hiyo leo tarehe 23 Februari, 2017

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...