Upatikanaji wake ni rahisi, wa haraka na ni huduma
salama ya kibenki kupitia mtandao

Benki ya Stanbic Tanzania imezindua huduma mpya ya malipo kupitia intaneti na simu za mkononi inayoambatana na huduma nyinginezo zinazolenga kuboresha ukusanyaji wa pesa na ufanyaji wa malipo kwa mashirika na biashara mbali mbali, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kutoa huduma rahisi na salama za kibenki

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma za Miamala wa Benki hiyo, Bw. Charles Mhina alisema mabadiliko hayo ya ufanyaji malipo na makusanyo yaani malipo ya pamoja kupitia internet na mitandao na uwekaji fedha benki – yatawahakikishia wateja wa benki katika sekta mbalimbali maboresho makubwa katika utoaji huduma

Akizindua huduma hiyo ya kipekee katika soko ijulikanayo kama Malipo ya Pamoja Kupitia simu ( Mobile Bulk Payment), Bw. Mhina alisema huduma hiyo itayawezesha mashirika kufanya malipo kutoka katika akaunti zao za Stanbic kwenda kwenye mitandao mbali mbali ya simu ikiwa ni pamoja na Tigo Pesa, Airtel Money,Mpesa na Ezypesa wakati wowote na popote walipo

Alisema Malipo ya Pamoja kupitia Simu yatatolewa kupitia mfumo wa utoaji huduma mtandaoni wa benki hiyo, ambao unawahakikishia wateja upatikanaji wa huduma wakati wowote, kwa njia rahisi, ya haraka na salama, jambo linaloongeza ufanisi zaidi katika ufanyaji wa miamala yao ya kibiashara.

“Uzinduzi wa huduma hii ni uthibitisho wa jitihada za Benki ya Stanbic katika kuboresha huduma zetu za ufanyaji miamala, lengo kuu likiwa ni kuleta tija katika biashara za wateja wetu,” alisema Bw. Mhina

Akizungumzia juu ya huduma ya malipo bila kutumia pesa taslim (Till to Bank Cashless Payment) ambayo itawawezesha wafanyabiashara kupokea malipo ya moja kwa moja kutoka katika mitandao ya simu, Bw. Mhina alisema huduma hiyo itaruhusu wamiliki wa akaunti za biashara kupokea malipo kupitia Mpesa, Tigopesa na Airtel Money kutoka kwa wateja wao kupitia namba maalum na fedha zitaelekezwa moja kwa moja kwenye akaunti zao za Benki za Stanbic

Alieleza kwamba kutokana na kuwa soko limetawaliwa na pesa taslim, huduma hii imelenga katika kupunguza mzigo mkubwa kwa wafanyabiashara wa upokeaji wa malipo ya fedha taslim na kubadilisha tabia ya wateja kwenda kwenye malipo ya mtandao

“Benki ya Stanbic ipo katika mstari wa mbele katika ugunduzi. Leo hii pia tunatambulisha huduma ya Till-to-Bank kwa wateja wetu. Malipo kupitia mtandao sasa yameyapita malipo ya pesa taslim na tunatizamia kuwa asilimia kubwa ya malipo hayatakuwa ya fedha taslim katika miaka michache ijayo. Tumesimama katika mhimili wa kulirahisisha hili kwa wateja wetu,” alisema.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma za Miamala wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Charles Mhina(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya malipo kupitia internet na simu za mkononi inayoambatana na huduma nyinginezo zinazolenga kuboresha ukusanyaji wa pesa na ufanyaji wa malipo kwa mashirika na biashara mbali mbali jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mkuu wa kitengo cha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, Allen Chiombola.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...