Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ.

Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limepania kukuza Mchezo wa Gofu kwa kujenga Miundombinu na Viwanja vya kanda katika maeneo mbalimbali nchini kwa Kuanzia Mkoani Dodoma ambapo Serikali imetangaza kuhamia.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati akifunga Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu Kuanzishwa kwa Klabu ya Golf ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam.
“ Tumeshapata eneo la Jeshi Dodoma hivyo Tutatumia uzoefu tulioupata kwa Ujenzi wa Klabu hii ili Kujenga Klabu ya Kisasa ya Gofu Mkoani Dodoma ili watakaokwenda Dodoma kikazi au kwa shughuli nyingine wasikose sehemu ya Kucheza Gofu.” Alisema Jenerali Mabeyo.

Aliongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Uwanja wa Golf Dodoma lakini pia kuna Uwezekano wa kujenga Viwanja vya kanda na Lugalo kuwa na mashina katika Mikoa ya Arusha,Morogoro,Mwanza na Simiyu ili kuchangia katika ukuzaji wa Michezo na ukizingatia Serikali imetilia Mkazo suala la Michezo kwa Wananchi.

Jenerali Mabeyo ambaye ni Mlezi wa Klabu hiyo alisema mbali na Ujenzi wa Viwanja hivyo vya Gofu lakini bado wataendeleza Uwanja wa Lugalo pale ambapo watangulizi wake wameishia na kuhakikisha unakuwa wenye sifa za kuchezeka wakati wote kwa kuangalia miundombinu ya Maji.

Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance mabeyo akikabidhi Zawadi kwa mshindi wa Jumla wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya  Gofu ya Lugalo Amani Saidi Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance mabeyo akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mrisho Sarakikya wakati akishiriki Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Mshindi wa kundi la Wanawake wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika Harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...