Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, akitoa hotuba ya kufunga Mafunzo
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya
nchini Marekani. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Wizara hiyo ambapo yalitolewa kwa Maafisa
Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka (hawapo pichani) kwa
kupewa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara
Haramu ya Usafirishaji Binadamu. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (kushoto), akipokea kitabu
kinachoelezea Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, kutoka kwa Jaji wa Mahakama Kuu
nchini Marekani, Virginia Kendall. Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without
Borders) ya nchini Marekani, waliandaa mafunzo kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi,
Mahakimu na Waendesha Mashtaka kwa lengo la kutoa uelewa na mbinu ya Kupeleleza,
Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu. Mafunzo
hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es
Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu nchini Marekani, Virginia Kendall, akizungumza na Maafisa Wapelelezi
wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka (hawapo pichani) kabla ya kufungwa
mafunzo ya kutoa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya
Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu kwa Maafisa hao. Mafunzo hayo yaliandaliwa na
Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani na
kuratibiwa na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya
Binadamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika
Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (kulia), Afisa wa Sekretarieti hiyo,
Happyness Laizer (wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa
Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani, mara
baada ya Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo yaliyotolewa kwa Maafisa Wapelelezi wa
Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka kufungwa. Mafunzo hayo yaliratibiwa na
Secretarieti hiyo na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es
Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...