Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemaliza kufanya ziara yake ya siku tatu katika jimbo la Shinyanga.

Katika ziara hiyo ya kikazi iliyoanza Februari 15,2017 kumalizika Februari 17,2017 ,Mheshimiwa Masele amekagua miradi ya maendeleo na kufanya vikao na wananchi wa kata 14 kisha kujadili na kuzitafutia ufumbuzi kero za wananchi. 

Katika maeneo mengi aliyopita,Mheshimiwa Masele amekutana na kilio kikubwa cha tatizo la njaa linalowakabili wananchi ambao walidai wamekuwa wakiendesha maisha yao kwa kunywa uji hivyo kuiomba serikali iwaone kwa jicho la huruma na kuwapatia chakula. 

Mheshimiwa Masele pia amekumbana na kilio cha bei kubwa ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA),huku wananchi katika maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria wakiomba huduma hiyo ili kuondokana na kero ya maji. 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiangalia eneo ambapo patajengwa choo kwa ajili ya shule ya msingi Twendepamoja yenye jumla ya wanafunzi 820 wanaotumia matundu 6 ya choo na walimu 8 pekee.Wa kwanza kushoto ni mwalimu Cephrine Philip anayefundisha katika shule hiyo. 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa amebeba mtoto katika ofisi ya mtendaji wa kijiji cha Seseko inayotumika kama Zahanati ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya kliniki kwa watoto .
Mheshimiwa Masele akiangalia choo kipya inachojengwa katika shule ya msingi Ushirika 
Mheshimiwa akiwa katika eneo la choo cha shule ambacho kinatumiwa na walimu na wanafunzi,eneo hilo ndipo pia patajengwa choo kipya 
Mheshimiwa Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Kizumbi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...