Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
Wasanii na
vikundi vinavyopiga muziki wa bendi wametakiwa kujitazama upya juu ya muziki
huo kutumika kama chombo cha kuuzia bia kwenye Bar.
Hayo
yamesemwa na msanii nguli wa muziki wa dansi hapa nchini John Kitime alipokuwa
akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habri katika jukwaa la sanaa
liliandaliwa na Baraza la Sanaa nchini (BASATA).
“Kuna vitu
tunafanya tunaona kama vya kawaida lakini ndio vinaua muziki wetu kama leo hii
bendi zinapiga kwenye bara kwa ajili ya kuuza bia na watu wanaangalia bure
hivyo inamaanisha bendi zetu ndio kichocheo cha kuuza pombe katika mabaa yote
mjini”amesema Kitime.
Kitime
ametoa wito kwa wasanii kuanza kubadilisha mtindo wa maisha kwani kitendo cha
bendi zote kuhamia kwenye bar ni moja ya anguko kubwa la muziki wa dansi nchini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...