Na Stella Kalinga, SIMIYU 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein ametimiza ahadi ya kutoa sadaka ya vifaa vya ujenzi wa Msikiti wa MASJID RAUDHAL  mjini Bariadi, ambao ni Msikiti mkuu Simiyu. 
Rais Shein alitoa ahadi hiyo mwezi Oktoba 2016 wakati alipokuwa Mkoani Simiyu kuwaongoza Watanzania katika Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl.Nyerere. 
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka amemshukuru Mhe.Rais Shein na kubainisha kuwa ujio wake mwaka jana umeleta mafanikio makubwa kwa mkoa na kujenga uhusiano mazuri kati ya Mkoa wa Simiyu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Mtaka amesema ujio wa Dkt Shein mkoani Simiyu umefungua milango ya ushirikiano wa kibiashara kati na Zanzibar, ambapo alimtuma Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe.Riziki Pembe Juma mwezi Desemba mwaka jana kuja kuona Chaki za Maswa na sasa Mkoa huo unauza chaki Zanzibar.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo,Mahamoud Kalokola (wa nne kushoto) na viongozi wengine wa BAKWATA mkoa wakipokea baadhi ya vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na Rais wa Zanzibar,Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein kukamilisha ujenzi wa msikiti wa MASJID RAUDHAL mjini Bariadi kutoka kwa mwakilishi wake Ally Habshy Abdallah
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya viongozi wa BAKWATA kabla ya kupokea vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na Rais wa Zanzibar,Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein ili kukamilisha ujenzi wa msikiti wa MASJID RAUDHAL mjini Bariadi kutoka kwa mwakilishi wake Ally Habshy Abdallah.
 Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola akizungumza na baadhi ya viongozi wa BAKWATA kabla ya kupokea vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na Rais wa Zanzibar,Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein ili kukamilisha ujenzi wa msikiti wa MASJID RAUDHAL mjini Bariadi kutoka kwa mwakilishi wake Ally Habshy Abdallah.
 Mwalikishi wa Rais wa Zanzibar,Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein Ndg. Ally Habshy Abdallah akizungumza viongozi wa BAKWATA kabla ya kuwasilisha vifaa vya ujenzi alivyovitoa kama sadaka yake ili kukamilisha ujenzi wa msikiti wa MASJID RAUDHAL mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akagana na  baadhi ya viongozi wa BAKWATA mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya ujenzi wa  Msikiti wa MASJID RAUDHAL mjini Bariadi kutoka kwa Rais wa Zanzibar,Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...