Asilimia 61 ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini hawana ujuzi na sifa za kuajiriwa kwenye sekta binafsi ili kukuza uchumi na kufikia kiwango cha kati .

Hayo yamebainishwa leo na Naibu waziri wa kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde wakati akizungumza na wadau wa makampuni ya sekta binafsi jijin Dar es salaam na kusema kuwa baada ya kugundua changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi wameanzisha mpango wa miaka 5 wa kuwasaidia vijana kupata mafunzo kwa vitendo ili kuongeza sifa ya kuajiriwa na kujiajiri.

''Tumeamua kuanzisha programu hiyo ili kuhakikisha wanasaidia nguvu kazi ya nchi kupata ujuzi wa kuweza kujiajiri lakini pia kuajiriwa katika makampuni mbalimbali yenye uhitaji wa wafanyakazi walio bora katika utendaji kazi" alisema Mavunde.

Mheshimiwa mavunde akaongeza kuwa programu hiyo ya miaka 5 iliyoanza mwaka 2016 na kutegewa kumalizika na kufikia mwaka 2021 unatarajiwa kuwafikia watu milioni 4 ili kuwasaidia kukuza ujuzi na kufikia uchumi wa kati kwa kuwepo nguvu kazi ya juu ya asilimia 34.
Naibu wazir wa kazi,vijana na watu wenye ulemavu Mh,Anthony Mavunde akizungumza na wadau Mbalimbali sekta binafsi katika mkutano uliohusisha serikali na sekta Binafsi uliozungumzia Mafunzo ya miaka mitano ya kuwapatia ujuzi wa kuajiriwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Mkurugenzi mtendaji Bw Godfrey Simbeye akitoa ufafanuzi katika Mkutano huo uliokutanisha Serikali na Sekta Binafsi
Baadhi ya Wadau waliohudhuria Mkutano huo leo Jijini Dar es salaam.Picha na Yasir Adam Blogu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...