KWAMBA TAREHE 08.02.2017 MAJIRA YA SAA 09:00HRS ASUBUHI, KATIKA MTAA WA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIAKANA KWA JINA LA JUMANNE NASSIBU MIAKA 20, MGOGO NA MKAZI WA MTAA WA MABATINI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA AKIMWINGILIA KIMWILI MBUZI JIKE, KITENDO AMBACHO NIKOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA 6:00HRS ASUBUHI  MMILIKI WA MBUZI  AITWAYE BENEDICTOR BUNGA MIAKA 33, MKAZI WA MTAA WA MABATINI, ALIKWENDA KUWAFUNGA MALISHONI MBUZI WAKE SITA KWA KUTUMIA KAMBA. AIDHA INASEMEKANA KUWA ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA TATU ASUBUHI (9:00HRS), MMILIKI WA MBUZI ALIKWENDA KUWACHEKI MBUZI WAKE ENEO ALIPOKUWA AMEWAFUNGA MALISHONI NA KUWAKUTA MBUZI WATANO BADALA YA SITA.
KUTOKANA NA KUKOSEKANA KWA MBUZI HUYO MMILIKI WA MBUZI HAO ALIPATWA NA HOFU HUKU AKIJUA MBUZI WAKE MMOJA AMBAYE HAMUONI ATAKUWA AMEIBIWA NDIPO ALIANZA KUTAFUTA VICHAKANI, GHAFLA  ALINADAI ALIMUONA MTUHUMIWA JUMANNE  NASSIBU VICHAKANI AKIWA ANAMWINGILIA KIMWILI MBUZI WAKE. INASEMEKANA KUWA MMILIKI WA MBUZI HUYO BAADA YA KUONA TUKIO HILO ALIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA NDIPO WANANCHI WALIFIKA NA KUMSAIDI KUMKAMATA MTUHUMIWA.
MTUHUMIWA YUPO POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA TUHUMA ZINAZOMKABILI YAKIENDELEA, PIA UTARATIBU UNAFANYIKA WA  KUPELEKWA MTUHUMIWA HOSPITALI,  ILI KUANGALIWA KAMA ANAAKILI TIMAMU,  PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA DHIDI YAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WAJIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU WENYE TABIA KAMA HIZO KWANI NI KOSA LA JINAI, ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.

IMETOLEWA NA.
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...