Na Bashir Yakub.
Kawaida hatimiliki( granted right of occupancy) hazitolewi kwa ardhi za vijijini. Ardhi za mijini tu ndizo huwa na hadhi ya kupata hatimiliki. Lakini wapo watu ambao wamechukua maeneo ya vijijni kwa ajili ya uwekezaji.
Wapo waliochukua ardhi kama wachimbaji wadogo, kilimo, madini, n.k. Hawa pengine wangependa wapate hatimiliki ili kukuza biashara zao sambamba na kupata faida zinazotokana na kuwa na hati miliki. Moja ya faida ya kuwa na hatimiliki ni pamoja na kupata mkopo.
Swali ni je inawezekana kuipatia ardhi yako ya kijijni hatimiliki yenye hadhi sawa na ile inayotolewa kwa ardhi za mijini?.
1.ARDHI YA KIJIJI NI IPI.
Sheria za ardhi namba 4 na 5 kwa pamoja zimeainisha aina tatu za ardhi kwa hapa Tanzania. Kwanza ardhi ya jumla, ardhi ya hifadhi, na ardhi ya kijiji. Ardhi ya jumla( general land) ni hii ardhi ya mijini ambayo huwa na hati miliki( right of occupancy). Hii ni asilimia 2 ya ardhi yote ya Tanzania.
Ardhi ya hifadhi( reserved land) ni kama mbuga, kingo za mito na bahari, makaburi, viwanja vya wazi n.k. Hii ni asilimia 28 ya ardhi yote. Ardhi hii huwa haimilikishwa labda isemwe vinginevyo.
Ardhi ya vijiji( village land). Hii ni ardhi ya vijiji kama jina lake lilivyo. Sote tunajua vijijini ni wapi. Inachukua jumla ya asilimia 70 ya ardhi yote.
2. UMILIKI WA WA AINA TATU WA ARDHI YA KIJIJI.
Ardhi ya kijiji iwe kwa uwekezaji, makazi au vinginevyo inaweza kumilikiwa kwa namna tatu tofauti. Kama ifuatavyo.
( a ) Kumiliki kwa haki bila nyaraka yoyote ya umiliki( deemed right of occupancy). Kwa mtu anayewekeza kijijini huu si utaratibu mzuri kwake. Hapa mmiliki atamiliki ardhi kijijini bila kuwa na nyaraka yoyote inayomtambulisha kama mmiliki lakini hilo halitamwondolea uhalali wake katika kumiliki. Wamiliki wengi vijijni humiliki kwa mtindo huu. Wengi wana ardhi lakini hawana nyaraka yoyote kudhibitisha kumiliki.
( b ) Kumiliki kwa hati ya kimila(customary certificate). Sura ya 114 sheria na 5 ya 1999 ya ardhi ya vijiji inatambua uwepo wa hati za kimila. Hati hizi hutolewa na halmashauri za vijiji kwa utaratibu maalum.
( c ) Kumiliki kwa hatimiliki( granted right of occupancy). Hatimiliki hutolewa kwa maeneo ya mijini tu lakini hata vijijini zinaweza kutolewa ikiwa ardhi inachukuliwa kwa ajili ya uwekezaji au shughuli nyingine za serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...