Wagonjwa wa Satarani wanaotibiwa katika
taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam
wataanza kunufaika na huduma bora kwa njia ya kisasa kwa kutumia Teknolojia ya
Mawasiliano kutokana na mchakato wa serikali kuimarisha huduma za taasisi hiyo.
Wakati jitihada hizo za serikali zinaendelea sekta
baadhi ya sekta binafsi zimeanza kuunga mkono jitihada hizo za serikali ambapo
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kupitia taasisi yake ya kuhudumia masuala ya
kijamii imetoa msaada wa kompyuta 10 za kisasa kwa taasisi hiyo.
Akiongea wakati wa kupokea msaada huo katika hafla
iliyofanyika hospitalini hapo leo,Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo,Dk.Julius
Mwaiselage,amesema kuwa msaada huu umepatikana katika kipindi mwafaka ambapo
hospitali hiyo iko katika mchakato wa kuendesha huduma zake kidigitali.
Dk.Mwaiselage alisema kuwa hivi sasa kumekuwepo na
ongezeko kubwa la wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa
uchunguzi na kutibiwa hivyo kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha kuwa ili
kuwahudumia ni kuwa na huduma za kisasa katika kila idara kwa njia ya TEKNOHAMA
na tayari serikali na wadau mbalimbali wameanza kufanikisha mchakato huo.
Aliishikuru kampuni ya Vodacom kwa kuwa mstari wa mbele
kuunga mkono jitihada hizo “Tunawashukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa
kuunga mkono jitihada za kuboresha huduma zetu ili ziweze kuwa bora zaidi na
tunatoa wito kwa taasisi nyingine kuendelea kutuunga mkono katika mapambano
haya ya kutokomeza ugonjwa wa Saratani nchini na kuwapatia huduma bora wahanga
wa ugonjwa huu”.Alisema.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa na misaada
mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa
wanaopata matibabu katika Taasisi ya Uchunguzi wa
Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam wakati walipowasilia
kwenye taasisi hiyo hivi karubni kutoa
msaada wa kompyuta 10 za kisasa kwa taasisi hiyo kupitia
kitengo chake cha Vodacom Tanzania Foundation. Msaada huo utarahisiha utoaji wa
huduma bora kwa angonjwa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom,Tanzania Jacqueline Materu
(kulia) na Mkurugenzi wa mawasilianao wa Wizara ya ujenzi ,Uchukuzi na
Mawasiliano ,Mhandisi Clarence Ichwekeleza (Kushoto) wakimsikiliza
kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uchunguzi wa Saratani
ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ,Dk.Julius Mwaiselage, wakati
alipokuwa akishukuru kwa Taasisi ya Vodacom Tanzania
Foundation kwa kuwapatia msaada wa Kompyuta 10 za
kisasa kwa ajili ya kusaidia kutao huduma bora kwa wagonjwa
wanaotibiwa katika Taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom,Tanzania Jacqueline Materu (kulia) , Mkurugenzi wa
mawasilianao wa Wizara ya ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano
,Mhandisi Clarence Ichwekeleza (wapila kulia ) na Meneja
ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Sandra Osward, (wapili kushoto) wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road jijini Dar es
Salaam ,Dk.Julius Mwaiselage,(kushoto) wakati alipokuwa akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya Komputa kati
ya 10 za kisas alizopewa msaada na Taaisi ya Vodacom Tanzania Foundation , kwa
ajili ya kusaidia kutao huduma bora kwa wagonjwa wanaotibia katika Taasisi hiyo
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom,Tanzania Jacqueline Materu (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road jijini Dar es
Salaam ,Dk.Julius Mwaiselage,(kushoto) moja ya kompyuta
kati ya 10 za kisasa zilizotolewa msaada na Taasisi ya Vodacom Tanzania
Foundation kwa ajili ya kusaidia kutao huduma bora kwa wagonjwa
wanaotibiwa katika Taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
'
Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa mawasilianao wa Wizara ya ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano
,Mhandisi Clarence Ichwekeleza (wapili kulia) na Meneja ruzuku na
Mawasiliano wa Vodacom Foundation Sandra Osward.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...