Walimu na wanafunzi wa shule za Msimbazi na Mongo la ndege ambao ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakijitolea kufanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya maadhimisho ya wiki ya utoaji huduma kwa wahitaji.
Wanachama hao walioongozwa na Mwenyeikiti wa chama hicho, Profesa Martha Qorro pamoja na Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba walifanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota na Ufukwe wa Coco.

Walimu na wanafunzi kutoka shule za Mugabe, Urafiki, Mongo la Ndege na Msimbazi ambao ni wanachama wa TGGA walishiriki ipasavyo kwenye usafi huo.
Pia baadhi ya wanachama wa TGGA walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Taifa cha Yatima cha Kurasini, Dar es Salaam.

 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Wanafunzi wa Shule za Mugabe na Urafiki na walimu wao wakifanya usafi katika Ufukwe wa Coco Oysterbay, Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha waiki hiyo ya utoaji huduma kwa wahitaji
 Wanachama wa TGGA wakifanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota
 Mwenyekiti wa TGGA, Profesa Martha Qorro (kushoto) na Juma Rashid wakiungana na wanachama wengine wa chama hicho kufanya usafi katika Ufukwe wa Coco, Oysterbay Dar es Salaam 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...