Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wasanii wa Sanaa ya uchoraji nchini wanataraji kufanya maonyesho ya wazi ya uchoraji katika bustani ya NBC iliyopo Posta ya zamani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kiongozi wa umoja wa wasanii hao wa kuchora, Amani Abeid amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuweza kuonyesha umma umuhimu wa sanaa za uchoraji katika majengo na ofisi za serikali.

“wachoraji wote maarufu hapa nchini na walioweza kufanya kazi nyingi za kimataifa watakuwepo hapo kuonyesha umuhimu wa sanaa hii ya uchoraji kwa taifa” amesema Abeid.

Kwa upande wake mchoraji vibonzo maarufu nchini , Nathan Mpangala amesema kuwa wasani hao kwa umoja wao watachora kasha baadae kufanya maonyesho ya picha hizo katika makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam

Nathani ametoa wito kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam kufika katika maonyesho hayo ambayo yataanza kuanzia saa 2 mpaka saa 6 mchana.
Mchoraji wa Vibonzo Nathan Mpangala akizungumza juu ya uwepo wake katika Tamasha hilo la uchoraji.
Kiongozi wa kundi la Wasanii wa Sanaa ya Uchoraji, Amani Abeid akizungumza na Waandishi wa habari juu ya maonyesho ya uchoraji katika eneo la bustani ya Posta ya Zamani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...