Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walimaji wa bustani katika bonde la mto msimbazi katika kata vingunguti iliyopo katika Manispaa ya Ilala, kuondoka mara moja na kuacha shughuli hizo.

Ameyasema hayo alipokua katika ziara ya siku moja ya kutembelea kata ya Vingunguti na kujionea athari mbalimbali za kimazingira katika kata hiyo.
Wakiongea mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamelalamika kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo bonde hilo kuzidi kumong'onyoka na kusogelea makazi ya watu pamoja na eneo la makaburi. 

Hivyo basi kusababisha nyumba zao kuanguka na makaburi kumong'onyoka hali amabayo inahatrisha maisha yao na kuwafanya kuishi kwa hofu.
Akijibu kero hiyo Waziri Makamba aliwaambia kuwa atayafanyia kazi maombi yao na atakaa na viongozi wa Manispaa na wa Ofisi yake ili kupata suluhu ya matatizo yao. 

Pamoja na hayo alisema kuwa kwa hatua za awali anawataka  wachimbaji na wakulima wa bustani kuacha mara moja shughuli hizo wanazofanya katika maeneno ya bonde hilo. (Habari na picha toka Kitengo caha mawasiliano Serikalini OMR)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia bonde la mto Msimbazi katika kata ya Vingunguti lilivyoharibika kwa shughuli za kila siku za Wananchi ikiwemo kilimo cha mbogamboga na uchimbaji wa mchanga. Waziri Mkamba yupo katika ziara kutembelea kata ya Vingunguti kukagua athari za mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bonnah Klauwa wakiskiliza kero mbalimbali zinazotolewa ana Wananchi wakati Mh. Waziri alipofanya ziara katika kata ya Vingunguti  kukagua athari mbalimbali za mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Wananchi waliojikusanya kumsikiliza wakati wa ziara yake katika kata ya Vingunguti katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipata maelezo, toka kwa vijana wa kata ya Vingunguti  juu ya utenegenezaji wa majiko ya mkaa ambayo ni rafiki wa mazingira na ambayo hayatumii mkaa mwingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...