KAMATI ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge ya Bunge la Jamhuri ya Uganda imetembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafao yanayotolewa na Mfuko kwa wanachama wake.

Ujumbe wa watu 6 kutoka nchini Uganda ulifanya ziara ya mafunzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Mfuko jana (28/3/2017) ambapo walipata fursa ya kuona na kuelezwa mbinu na mafanikio ya Mfuko huo.

Wabunge hao ni pamoja na Amos Lugoloobi (Mb), Muwanga Kivumbi (Mb), Kaberuka James (Mb), Felix Kaluyigye (Mb), Opolot Isiagi (Mb) na Ofisa wa Ubalozi wa Uganda nchini Tanzania Doroth Kalema.

Akiukaribisha ujumbe huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda alisema kuwa Mfuko unajisikia faraja kubwa kupata ugeni huo ambao umetambua kazi kubwa inayofanywa na NHIF na kuona umuhimu wa kufika na kujifunza ama kupata uzoefu wa namna ya utekelezaji wa shughuli hasa za utoaji wa mafao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko Bw. Bernard Konga alitaja makundi yanayohudumiwa na Mfuko kuwa ni pamoja na Waajiriwa wa sekta rasmi, Kampuni binafsi, wanachama binafsi, wajasiliamali, watoto chini ya umri wa miaka 18, wanafunzi pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini.

“NHIF imefanikiwa kuwa na mtandao mkubwa wa vituo vya kutolea huduma ambapo kwa sasa ni zaidi ya vituo 6,000 na mafao wanayopata wanachama ni mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yanaondoa usumbufu wote wakati anapopata ugonjwa,” alisema Bw. Konga.

Kwa upande wa ujumbe huo waliupongeza Mfuko kwa kazi kubwa inayofanya lakini pia kwa ushirikiano ambao imekuwa ikionesha kwa nchi yao wakati wowote wanapokuwa na nia ya kuja kujifunza.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga akitoa uzoefu wa huduma za Mfuko kwa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Uganda ambao walitembelea kwa lengo la kupata uzoefu. Kati kati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda.
Wabunge wakipata maelezo katika Kituo cha Huduma kwa Wateja cha NHIF.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda akiwa na wageni katika picha ya pamoja.
Wageni wakiagana na Mwenyekiti wa Bodi Mama Anne Makinda baada ya kumaliza ziara yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...