Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama leo imefanya ziara ya kukagua mradi wa Vitambulisho vya Taifa; ambapo mbali na kupokea taarifa ya utekelezaji pia walitembelea na kukagua kituo kikuu cha Kuhifadhi, kuchakata na kuzalisha Vitambulisho vya Taifa -Data Centre.

Akizungumza wakati wa kukaribisha Kamati hiyo; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema mpaka sasa NIDA imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa kiwango kikubwa pamoja na changamoto kubwa ya fedha iliyopo.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati hiyo; Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Adad Rajab (Mb) amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na NIDA na kwamba Kamati imeridhishwa na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na NIDA na kwamba Kamati yake itaendelea kuishauri Serikali kuongeza bajeti ya fedha kwa NIDA ili kuwezesha kukamilisha zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa, kwani manufaa ya kuwa na mradi huu kwa Taifa ni makubwa katika Nyanja zote.

Wakitoa maoni yao wajumbe wa Kamati hiyo wameitaka Wizara kuiwezesha NIDA na kuharakisha matumizi ya Vitambulisho vya Taifa kielektroniki kwani tayari idadi kubwa ya wananchi wameshatambuliwa na taarifa zao kuingizwa kwenye mfumo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama walipowasili NIDA kutembelea na kukagua maendelea ya mradi wa Vitambulisho vya Taifa.

Nje, Ulinzi na Usalama Mh. Adad Rajab (Mb), akiongea jambo wakati wa kikao na Menejimenti ya NIDA baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. Andrew W. Massawe. Kulia ni Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Kanali Mstaafu Ramadhani Issa Abdallah(Mb).Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew W. Massawe, akisoma ripoti ya Utekelezaji Mradi wa Vitambulisho vya Taifa kwa kamati ya ulinzi na Usalama ya Bunge. Kushoto ni Mh Sophia H. Mwakagenda(Mb) na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi Mh. Balozi Simba Yahya.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge wakisikiliza jambo wakati walipotembelea kituo cha uchakataji taarifa cha NIDA (NIDA DATA CENTER). Katikati ni Mh. Adad Rajab(Mb) mwenyekiti wa kamati na kulia ni Mh. Sophia H. Mwakagenda(Mb) Mjumbe wa kamati


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...