Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah  Kairuki amesema kwamba serikali itahakikisha kwamba Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) tawi la Mbeya kinakuwa na majengo yake ili kupunguza gharama za uendeshaji.
Kwa sasa chuo hicho kinatumia majengo ya kukodi ambayo ni mali ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya,majengo hayo yapo eneo la  soko Matola, Chuo kinahudumia wakazi wa Nyanda za Juu Kusini.
Akiwasilisha taarifa ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania tawi la Mbeya mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge  Utawala na Serikali za Mitaa  Waziri Kairuki alisema gharama ya kodi ya shilingi milioni 24 kwa mwezi ni kubwa na kwamba serikali iko katika mchakato wa kuhakikisha kwamba chuo hicho kinamilikishwa mjengo hayo ili kupunguza gharama za uendeshaji.
 Aidha Waziri huyo alisema kwamba serikali itahakikisha kwamba chuo kinakuwa na wakufunzi wa kutosha ili kuendesha kozi zake kwa ufanisi.
Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo aliiambia kamati hiyo kuwa tawi la Mbeya linakua kwa kasi kwani kwa sasa lina wanafunzi 1236, tawi hilo lilizinduliwa mwaka 2014 likiwa na wanafunzi 453.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  Utawala na Serikali za Mitaa  Mhe. Jason Rweikiza akizugumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo hawapo pichani katika Ukumbi wa chuo hicho Jijini Mbeya, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah  Kairuki, kulia ni Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo. Picha na Kenneth Ngelesi
Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Tawi la Mbeya Dk. Heriel Nguvava katikati akiwaonyesha chumba cha Kompyuta wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  Utawala na Serikali za Mitaa  walipofanya ziara chuo hapo kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jason Rweikiza kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah  Kairuki. Picha na Kenneth Ngelesi. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...