Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Watanzania wenye vipaji wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza na wamewataka wajitokeze kwa wingi katika mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa na Mtanzania Emanuel Houston anayeishi Nchini Ujerumani.

Emanuel ameambatana na baba yake Luis Houston ambao wote wanaishi nchini Ujeruami na wataendesha mafunzo hayo kupitia taasisi ya Unleashead Academy iliyo chini ya Halila Mbowe.

Akizungumza na waandishi wa habari, Emanuel amesema kuwa anafurahi kuja kuwafundisha vijana wa kitanzania namna ya kucheza na watapata fursa ya kumuuliza kitu chochote.

Emanuel amesema kuwa, kuja kwake nchini Tanzania anategemea kuona vijana wengi kuja kujifunza kwani katika nchi za Ulaya watu wanaanza kujifunza mapema zaidi wakiwa na umri mdogo ndiyo maana wanaweza kufika mbali katika sekta mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed Academy Halila Mbowe amesema wanafuraha sana kuweza kuwakaribisha vijana katika kituo chao na pia kushirikiana na Emanuel Houston pamoja na Ben Pol kuja kuandaa mafunzo hayo kwa vijana.

Halila amesema kuwa kituo chake kinajihusisha na masuala ya kuinua vipaji katika kucheza mziki na kuandika mashairi na wameweza kupata vijana wengi na na takribani 25 tayari wameshaingia katika mashindano makubwa.

Baba yake na Emanuel, Luis Houston amesema kuwa alianza kukijua kipaji cha mwanae toka alivyokuwa mdogo na akamwambia kuwa utakuja kuwa mcheza mziki (dancer) na kweli mpaka sasa ameweza kuendesha maisha yake kupitia kucheza na ameshafungua kituo cha mafunzo nchini Ujerumani na ana wanafunzi takribani 15000.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwa kesho katika studio za Unleashead zilizopo Mikocheni B na itaanza saa 9-11 alasiri na hakutakuwa na kiingilio chochote.

Mtanzania Emanuel Houston akizungumza na waandushi wa habari kuhusiana na mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa nae hapo kesho chini ya Unleashed Academy, kushoto ni msanii na mratibu wa mafunzo hayo Bernad Paul 'Ben Pol' na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed 

Academy Halila Mbowe.


Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed Academy Halila Mbowe akizungumzia jinis kituo chake kinavyofanya kazi katika kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania katika kucheza na kutunga mashairi, Kulia ni Luis Houston ambaye ni baba yake na Emanuel Houston (wa pili kushoto) na 



 msanii na mratibu wa mafunzo hayo Bernad Paul 'Ben Pol' 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...