KUZ: 27.01.1943 – KUF: 28.03.2016
Leo tarehe 28 Machi, 2017 umetimiza mwaka mmoja kutoka ulipotuacha na kwenda kwa Muumba wako. Hatuna maneno yanayoweza kuelezea majonzi na huzuni ya kuagana nawe lakini kumbukumbu yako itaishi nasi siku zote. 
Tunakumbuka upendo wako usio na ubaguzi, utu wako na ukarimu wako ambao ulimfanya kila aliyekufahamu kuguswa kipekee.
Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa  kutujalia kuwa na mama kama wewe kwa muda wote tulioishi nawe hapa duniani. Unakumbukwa daima na mume wako mpenzi Mzee Stephen Philip Assey, watoto wako ,wajukuu zako, majirani zako, ndugu, jamaa na marafiki.
Misa  ya kumwombea  marehemu mama yetu mpendwa  itafanyika katika Kanisa Katoliki la Mt Martin De Porres lililopo Mwananyamala tarehe  2 Aprili 2017, saa 3.00 kamili asubuhi.


                                   Ufunuo 14:13b Heri Wafu wafao katika Bwana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...